Ndoa

KWENU WOTE MLIO KWENYE MCHAKATO WA KUTAFUTA WACHUMBA..!!
Sababu kubwa ya Mungu kumuumba mwanamke ilikuwa ni kumpatia mwanaume msaidizi wa kufanana nae. Neno hili, “Wa kufanana nae” linaeleweka zaidi unaposoma kwenye Biblia za Kiingereza ambapo ni, “Fit for Him” na “Meet For Him”. (Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ‘Wa kukamilishana nae’). Kuna kitu cha kuelewa hapa: Kwa mujibu wa Mithali 30: 11-14, Mungu ametuumba wanadamu wa makundi takribani manne. Biblia inayataja makundi... haya kama, “Temperaments” (Yaani namna Mungu alivyowaumba watu kiutofauti kutegemea vipawa vyao, udhaifu wao na ubora wao); ambapo wanasaikolojia wameyapa majina ya kitaalamu zaidi; Melancholic, Phlegmatic, Sanguine na Choleric. Kila kundi hapa lina tabia za kiasili katika tendo la ndoa, katika fedha, katika malezi, katika uvumilivu, katika mitazamo, katika imani, kihisia n.k. Unapochumbia ama kuchumbiwa; hutakiwi kukurupuka, hutakiwi kumpenda ama kumkubalia kila anaetangaza nia. Kijana wa kiume unatakiwa ujitambue wewe ni wa kundi lipi ndipo unakuwa na wasaa mzuri wa kuchagua msichana kutoka kundi “Fit for You” ambalo “Mtakamilishana”. Hii ya kujitambua na kutambua mwenzi wa kundi gani umchague, sio kazi ya Mungu, ni kazi yako kwa sababu Mungu alishamaliza kazi ya kuumba na ameshakukabidhi akili, ufahamu na amekutaka utafute maarifa ili usiangamie. Usije ukamlaumu Mungu huko mbeleni, utakapoingia mkenge wa kuoa ama kuolewa na mtu ambae badala ya “kukamilishana” mkajikuta “mnabomoana”, badala ya ubora wa mmoja kufunika udhaifu wa mwingine, mkajikuta mmetengeneza bwawa la madhaifu ndani ya nyumba. Mathalani: Wanaume wa kundi la Melancholic kiasili hawana ‘emotions’ kali na za mara kwa mara katika tendo la ndoa na katika issue ya fedha na matumizi ni wabahili sana. Wanawake wa kundi la Sanguine wako ‘very active’ katika tendo la ndoa na emotions zao ni kali na za mara kwa mara na katika issue ya fedha ‘hawanaga’ breki katika matumizi. Sasa ikitokea Mwanaume Melancholic amemuoa mwanamke Sanguine; ndoa hiyo Mungu asipoingilia kati ni majanga-kwa sababu uwezekano wa mwanamke kuisaliti ndoa ni mkubwa na migogoro ya kiuchumi ni suala la kupigia mstari hapo. Nafahamu wapo wengi wanaooana kwa kubahatisha (na Mungu anawasaidia wanapatiana makundi sahihi); lakini wewe ambae upo kwenye mchakato wa kutafuta mchumba nakushauri usienende kwa kubahatisha. Tafuta maarifa ukawe salama katika ndoa yako unayoitarajia

0753 391634

No comments:

Post a Comment