Saturday, February 8, 2014

Jehanum ya Moto ni Wapi na Kukoje?

Miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa nimezama sana katika dhambi. Nilipokuwa katika lindi hilo la dhambi, sikutaka kusikia chochote kwa mtu yeyote aliyenieleza kwamba niache dhambi, na eti niokoke. Niliwaona watu wanaohubiri mambo ya kuokoka, wameshindwa maisha, wamechanganyikiwa (frustrated), na tena

hawajasoma . Nakumbuka siku moja, mhubiri mmoja alinihubiri na kuniambia, ”Acha dhambi, au sivyo utatupwa katika Jehanum ya moto.“ Unajua nilimjibuje! Nilimwambia, ”Wewe usinibabaishe na hiyo Jehanum ya moto. Potelea mbali nikienda motoni, pilipili usizozila zakuwashia nini? Usinifuatefuate katika maisha yangu, chukua ”time“ yako!

Baada ya miaka kadhaa kupita, nilipokuja kusikia mafundisho kuhusu jinsi kulivyo huko Jehanum ya moto, nilikuja kufahamu kwamba yule mhubiri nilimjibu ”potelea mbali nikienda motoni“, kwa sababu tu sikuwa ninaelewa lolote kuhusu jinsi Jehanum kulivyo; kwa kuwa sikuwahi kufundishwa mafundisho hayo na kiongozi

wangu wa dini. Tangu niliposikia mafundisho hayo, maisha yangu yalibadilika kabisa. Mpendwa msomaji, huenda hata wewe hujasikia mafundisho halisi kuhusu jinsi kulivyo Jehanum ya moto, kama mimi nilivyokuwa; ndiyo maana nimeona leo nikushirikishe mafundisho haya kupitia katika tovuti hii. Mungu akubariki kwa kuendelea kusoma ujumbe huu.

Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu. Tunasoma katika WAEBRANIA 9:27, ”Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.“ Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya Neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu anapokufa, analala

tu, na hakuna lolote la hukumu mara moja wakitumia maandiko yafuatayo na kuyatafsiri visivyo: MATHAYO 27:52; 1WAKORINTHO 15:20: YOHANA 11:11-14 n.k.; na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu. Roho ya mtu huondoka na kuingia katika mwili mwingine, unaoitwa mwili wa roho Miili tuliyo nayo wanadamu kabla ya kufa, inaitwa miili ya asili. Tunasoma katika 1WAKORINTHO 15:40, 44, ”Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, …Ikiwa uko mwili wa asili, na wa r oho pia uko.“

Mwili wa asili, ndio unabaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka kama tunavyosoma katika MHUBIRI 12:7, Nayo mavumbi ya nchi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.“Mwili wa asili, ndio unaobaki kaburini, na huo ndio unaotajwa kwamba umelala, haujui lolote, na hauna kumbukumbu; lakini pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu na kukabiliana na hukumu yake dakika ileile baada

ya kufa (AYUBU 19:26). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa mbinguni (LUKA 23:43; 16:22). Ikiwa ameishi na kufa katika dhambi, bila kutubu dhambi zake na kuokoka, hukumu yake mtu huyo, huwa ni kutupwa katika Jehanamu ya moto, mara tu baada ya kufa, kama yule tajiri anayetajwa katika Biblia (LUKA 16:19-24).

Mbinguni ni juu (Mbingu ya tatu), lakini kuzimu au Jehanamu ya moto, ni pande za chini zanchi (2 WAKORINTHO 12:1-4; MITHALI 15:1-4; MITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14. Mara mtu anapokufa, hufika kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni kuzuri, hata hivyo ikiwa jina lake haliko katika kitabu

cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni, huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni. Hali hii wakati mwingine inaweza kuonekana katika mwili wa asili kwa kumwangalia mtu anavyotapatapa na kuhangaika sana katika kufa kwake. Kutokana na mtu asivyopenda kwenda motoni na kutaka kwenda mbinguni asikotakiwa, mtu hulazimika kukamatwa kwa nguvu na malaika wa kutisha, na kutupwa katika Jehanum ya moto; inayojulikana pia kwa jina jingine, giza la nje; kama

tutakavyoona baadaye kidogo (UFUNUO 19:20; 20;10; MATHAYO 25:30).

Huko motoni Jehanum kukoje? Kunatisha, nashindwa hata nikueleze vipi unielewe. Moto wa milele, hatukuwekewa wanadamu bali shetani na malaika zake (MATHAYO 25:41). Kama utakwenda huko baada ya kusoma ujumbe huu, itakuwa ni kwa sababu ya kiburi chako tu, na kushupaza shingo yako na kukataa kulitendea kazi Neno hili (MITHALI 29:1). Moto wa Jehanum siyo mahali pa mchezo kama walimu wa uongo wanavyofundisha. Waalimu hawa huwafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa na kuangamizwa kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 (kuangamizwa) na YOHANA 3:16 (kupotea). Kuangamia katika maandiko hayo haimaanishi kumalizika kabisa, bali kukabiliwa na mauti (ESTA 4:16). Mauti ya watu walioko motoni, ni mauti ya milele, kama tutakavyoona hivi punde. Kondoo akipotea, haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (ISAYA 57:1-3).

Vilevile, neno ”Kuharibu“ linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele, halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni kuadhibu vikali (1WAKORINTHO 3:16-17. Waalimu hawa wa uongo, pia hufundisha pia kwamba, eti watu watatoweshwa kama moshi baada ya kuunguzwa kwa kutumia andiko la ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni

kutenganishwa na Mungu, kama Adamu na Hawa walivyotoweshwa na kutolewa katika bustani ya Edeni, na hivyo kutengwa na Mungu, Kwa ujumla, mafundisho yote haya yanayotokana na Shetani, yanalenga kuwafanya watu waendelee kutenda dhambi, huku wakipuuza ukweli juu ya Jehanum, kwa kuwaza kwamba watateseka dakika chache na kupotea kabisa na ndiyo mwisho. Hiyo siyo kweli.

Ukweli kuhusu Jehanum ya moto ni upi basi? Sikiliza nikuambie! Jehanum ya moto, au Kuzimu, ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Wengi tunafahamu jinsi wanawake wanavyouchochea moto wa kuni au mkaa, kwa kuupulizia hewa kwa mdomo, au kipepeo. Sasa basi, moto wa Jehanum nao huchochewa mfululizo, ili usizimike; lakini huchochewa na pumzi ya Bwana, yaani pumzi maalum ya Mungu mwenyewe (ISAYA 14:15; 30:33). Moto wa Jehanum ni mkali sana kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani. Moto wa gesi wa kuunganishia vyuma, unaotokana na kuwashwa mchanganyiko wa gesi ya ”Oxygen“ na ”Acetylene“, moto huu unaonekana kwa hapa duniani kwamba ni mkali. Moto huu, siyo chochote, ukilinganishwa na moto wa Jehanum. Katika karakana au viwanda vinavyotengeneza vifaa vya chuma, chuma huyeyushwa na kuwa ujiuji katika matanuru ya moto mkali unaofikia nyuzi joto 2,000 hadi 3,000 na zaidi. Moto huu unaoyeyusha vyuma na ukali wake, huo si chochote! (Kumbuka kwamba maji yaliyochemka sana hufikia nyuzi joto 100 tu!). Moto ulio katikati ya jua linalotuangaza, unafikia nyuzi joto milioni kumi . Moto wa jua nao, si chochote ukilinganishwa na moto wa Jehanum! Ukali wa moto wa Jehanum, unatisha (WAEBRANIA 10:26-27). Siyo hilo tu, moto wa duniani una rangi mbalimbali, njano, bluu, nyekundu n.k. Moto wa Jehanumu ni tofauti kabisa; Ni moto wa rangi nyeusi, unaosababisha giza na kumfanya mtu aliye motoni, awaone wenzake wachache tu wa karibu naye, hivyo hamna faraja ya kusema ”tuko wengi!“ Moto huu mweusi, ndiyo maana unaitwa ”giza la nje“ Mathayo 8:11-12, 22:13; 25:30; YUDA 1:6). Siyo hilo tu. Moto huu wa Jehanum, una meno! Hivyo una uwezo wa kuwala na kuwatafuna walioko motoni (KUMBUKUMBU 32:22; WAEBRANIA 10:26-27). Hata hivyo, pamoja na moto huu kumtafuna mtu, bado una sifa ya kumhifadhi mtu huyo na kumfanya asimalizike, kama jinsi chumvi ilivyo na uwezo wa kuizuia nyama kuharibika. Hivyo moto unamtafuna mtu wakati wote, lakini haishi na wala moto wenyewe hauzimiki. Ndiyo maana unaitwa moto wa milele (MARKO 9:43-49; MATHAYO 25:41).

Moto huu wa Jehanum, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaaluma, Sulphur.“ Kwa wale wanaofahamu kidogo somo la shule la ”Kemia,“ au ”Chemistry,“ wanafahamu kwamba madini ya ”sulphur“ yakiwashwa moto, huwa kama mpira, na hutoa harufu mbaya kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii

inafunika kuzimu yote, na watu walioko huko wanahangaika kushika pua zao, lakini hakuna jinsi! Hebu jaribu kuwaza maisha haya, ndiyo yawe ya milele, mpendwa msomaji! Siyo hilo tu! Katika moto huu, wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi makubwa katika miili yao, wakiingia na kutoka, kutoka ubavu hadi ubavu mwingine, kutoka kwenye tumbo hadi mgongoni n.k. Hii hufanya sura za wale walioko motoni, kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Hata kama mtu alikuwa mweupe duniani, huko motoni, huwa ni mweusi tii!

Moto wa milele, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Kwa nini huitwa mauti ya pili? Uchungu wa mauti unaomfanya mtu kugugumia kwa mateso makali, akishindwa kupumua vizuri na kubaki kusema ”Mmh! Mmh! Mmh!, mpaka watu wanasema heri afe apumzike, uchungu wa jinsi hiyo humkabili mtu aliye motoni, milele na

milele. Kwa lugha rahisi, ni kusema kwamba watu walioko motoni, wakati wote wako katika hali ya kufa, lakini hawafi! Niseme nini ili unielewe! Watu walioko motoni, hujawa wakati wote na vilio, na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali (MATHAYO 8:12). Walioko motoni wanajifahamu, na kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani, na tena wakati mwingi hutoa ndimi zao nje, kama mbwa, wakitamani maji kidogo kupoza ulimi kutokana na joto kali linalosababisha kiu kubwa, lakini hawapati maji hata tone! Juu ya yote hayo katika vilio vyao, humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, Nami jicho langu

halitaachilia, wala sitaona huruma (EZEKIELI 9:10; 8:18).

Watu walioko motoni, hutamani mtu mmoja kati yao atoke motoni aje duniani, awashuhudie ndugu zao, ili waache dhambi, na kukwepa mateso yao, lakini huambiwa kwamba ndugu zao wanapaswa kuyasikia maneno ya manabii walioko duniani, maana hata akitumwa mtu kutoka motoni na kuelezea mateso ya huko, watasema ni mwongo, hajaenda motoni. Tunasoma haya katika LUKA 16:27-31, ”Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali

hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, wanao Musa na manabii, wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea watu atokaye kwa wafu, watatubu. Akawaambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa (hawatashawishika) hata mtu akifufuka katika wafu.“

Mpendwa msomaji, ikiwa mama yako mzazi alifariki akiwa hajaokoka, ujue yuko motoni, na anakuambia, ”Usinifuate huku mwanangu“. Ikiwa baba yako mzazi alifariki akiwa dhambini, anateseka motoni, na hataki umfuate huko aliko! Ndugu, marafiki na jamaa zako walioko huko wanakukumbuka sana, na hawapendi ujiunge nao huko,

bali wanataka utubu na kuokoka mateso hayo ya moto. Walioko huko motoni, wakimwona yeyote mwingine kutoka duniani, ambaye alikuwa na nafasi ya kusikia habari kama hizi na akazipuuza, kisha akawafuata huko motoni, humwambia, ”Je, wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!“(ISAYA 14:10).

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka. Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2WAKORINTHO 6:2). Labda unajiuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi. Kwa imani ukitubu dhambi zako huku ukimaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari.Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni,



”Mungu Baba asante kwa kuniletea ujumbe huu. Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu. Amen. Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika utakwenda mbinguni, hata ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Friday, February 7, 2014

SABABU SABA ZA KIBIBLIA KWA NINI WATU WANAKUFA MAPEMA


Bwana Yesu asifiwe sana wana wa Mungu, ni matumaini yangu na Imani yangu ya kwamba u mzima na ya kuwa unaendelea kuufurahia uzuri wa Yesu Kristo na kazi yake ya msalaba.
 Leo ninataka kwa pamoja tuyachunguze maandiko na tuzipitie sababu hizi saba za Kibiblia ni kwa nini watu wengi wanakufa mapema...na sasa ongezeko la vifo vya mapema ni kubwa kuliko hata zamani. Kwa Tanzania wastani wa kiwango cha maisha ni miaka 45,Binafsi nauona umri huu kuwa ni mdogo sana kwa mtu wa rika hili kuondoka duniani kwani anakuwa na majukumu mengi ya kufanya na pia mchango wake unakuwa unahitajika kwenye familia, ukoo, wilaya, mkoa, taifa na hata duniani kwa ujumla.
 Ni maombi yangu na dua yangu kwa Bwana ya kwamba umalizapo kusoma ujumbe huu, macho yako ya ndani yatafunguka na utaweza kuona swala hili kwa jicho la Rohoni...KARIBU SANA.
                Zifuatazo ni sababu saba kwa mujibu wa Neno la Mungu ni kwanini watu wanakufa mapema(katika umri mdogo)
 1.KUTOWAHESHIMU WAZAZI(BABA NA MAMA)
 Biblia iko wazi sana na imesisitiza uhusiano mzuri na wa uhakika kati yetu na wazazi wetu...kinyume chake LAANA zitayaandama maisha yetu na maisha yetu hayatakuwa ya heri na marefu.
 Ukisoma Waefeso 6:1-3 inasema, "Enyi watoto watiini WAZAZI wenu katika BWANA, maana hii ndiyo HAKI.Waheshimu baba na mama yako, amri hii ndiyo ya kwanza YENYE AHADI (za ustawi, baraka na wingi wa miaka), upate HERI, UKAE SIKU NYINGI( UISHI SIKU NYINGI) katika dunia"   pia katika Kumbukumbu la Torati 5:16 Biblia inasema, "Waheshimu BABA na MAMA yako; kama BWANA, Mungu wako alivyoamuru, SIKU ZAKO ZIPATE KUZIDI, nawe upate KUFANIKIWA katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako"
 Kwa mujibu wa maneno ya Mungu hapo juu ni dhahiri kabisa ya kuwa watu wote wasiowaheshimu wazazi wao, ni ngumu kufanikiwa, Laana zinawafuatilia na zaidi ya yote wana muda mchache wa kuishi...WANAKUFA MAPEMA!
 2.KUKOSA MAONO
  Kwa mujibu wa Biblia, mtu anayeishi ili mradi tu, asiyejua kwanini yupo duniani, asiyekuwa na kusudi na mpango katika maisha yake, na asiyeweza kupanga hata mipango ya 'kesho nitafanya a, b, c nk' yuko katika hatari kubwa ya kuondoka duniani kabla ya muda wake...Biblia inasema, "Pasipo MAONO watu huangamia"....Biblia ya kiingereza inasema, "Without VISION people PERISH"
 Jitahidi kuwa na maono ya muda mfupi na ya muda mrefu, Mungu anashughulika na walio nacho, wasiokuwa nacho hata kile kidogo walichonacho hunyang'anywa.
 3.KUTOKUMCHA MUNGU
 Kumcha Mungu ni kuishi maisha yanayoongozwa na HOFU ya MUNGU (si woga dhidi ya Mungu)...Ni maisha ambayo moyo,mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejawa na kiu na njaa ya kumpendeza Mungu na kuyafanya maagizo yake yote-tena kwa furaha.
 Mithali 10:27 inasema, "KUMCHA BWANA kwaongeza siku za mtu, Bali miaka yao WASIO HAKI itapunguzwa"  na pia Mhubiri 7:17 inasema, "Usiwe MWOVU kupita kiasi; wala usiwe mpumbavu; kwanini UFE KABLA YA WAKATI WAKO?"
 Kwa mujibu wa ushahidi huu wa Neno la Mungu, ni dhahiri kuwa maisha yasiyo na uchaji na yasiyoongozwa na hofu ya Mungu, yanawafanya wengi wafe kabla ya muda wao waliokusudiwa kuishi.
 4.KUMWEKEA MUNGU MIPAKA
 Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi...kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni 'DHARAU' kwake... Zaburi 78:41 inasema, "Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel"
 Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.
 Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya 'Maziwa na Asali'...10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki...majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema...waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni 'UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO' wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi...WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO...Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)
 Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako...ishi maisha ya IMANI...Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, "Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia" Isaya 55:8-11
 5.KUTOKUMTUMIKIA MUNGU
 Biblia inasema katika KUTOKA 23:25-26, " Nanyi  mtamtumikia BWANA, Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; NAMI nitakuondolea Ugonjwa kati yako...na  hesabu ya SIKU zako nitaitimiza"
 Huu ni ukweli ambao inabidi uufahamu na uweke kwenye matendo.Unataka kuishi muda mrefu hapa duniani? kazi ni rahisi...fanya sehemu yako, MTUMIKIE BWANA naye ATAITIMIZA hesabu ya siku zako...HAUTAKUFA KABLA YA WAKATI.
 6.MAISHA YA DHAMBI
 Dhambi ni mbaya...inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako...inakufanya ufe kabla ya muda wako...Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako...unafanya kazi ambayo mshahara uitwao 'MAUTI' utaupata.
 Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, "Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu"  pia Biblia inasema, "Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa"
 Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi...Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?
 Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!
 7.KUKOSA BIDII KATIKA KUMPENDA MUNGU
 Biblia iko wazi katika Zaburi ya 91:14-16, nayo inasema, "Kwakuwa AMEKAZA(Ameweka bidii katika) KUNIPENDA, Nitamwokoa; na kumweka palipo juu (NITAMWINUA) kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni. Nitamwokoa na kumtukuza; KWA SIKU NYINGI nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu"
 Biblia inasema Atakayekaza/kuwa na bidii katika KUMPENDA MUNGU atashibishwa kwa WINGI WA SIKU.
 Yesu ameweka wazi ni namna gani waweza kumpenda Yeye, Yohana 14:21 inasema, "Yeye aliye na AMRI  zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; Nami nitampenda na kujidhihirisha kwake"
 Nayo Mithali 3:1-2 inasema, " Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike AMRI zangu.Maana zitakuongezea WINGI WA SIKU, NA MIAKA YA UZIMA, NA AMANI"
 Unapozishika sheria na Amri alizozitoa Bwana maishani mwako...huo ndo udhihirisho wa Upendo wako kwa Mungu aliye hai...kila unapoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu Mungu-ukakaza kumpenda, ANAKUSHIBISHA KWA SIKU NYINGI...Wewe ndiye unayeweza kumwambia Bwana, hii miaka 90 inatosha, nimekwisha shiba maisha...nataka kurudi nyumbani...au miaka 40 inatosha Bwana...nimeshiba siku nataka kurudi nikae na wewe...wewe ndo unayeamua wingi wa siku zako...tangu leo kaza kumpenda BWANA.
               Ninaamini umejifunza kitu, na ya kuwa wewe nawe utayagusa maisha ya wengine kwa KWELI hizi ambazo Bwana amesema na wewe kupitia kwangu.Ubarikiwe
    Wako katika na Ndani ya Kristo

Kwa Viumbe Vyote Barabara 13


Bwana Ndiye Mchungaji.


Mwili wako ni Hekalu la Mungu!

1 KOR. 6:18-19

Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

Wako wapi mabinti/wakaka wanaomuheshimu MUNGU…Unapopiga picha za utupu na kuweka mitandaoni siyo kwamba unawaburudisha watu la! hasha bali unajishushia thamani wewe. alafu unamkosea MUNGU kwa sababu Mwili wako ni HELAKU,mwili ni Nyumba iliyovaa ROHO…MUNGU alikufinyanga akakutengeneza ili uje Duniani…Yaani wewe asili yako ni MBINGUNI…..Wanadamu wote walitoka mbinguni, na asili yetu ni mbinguni kwa Mungu. Hata ukisoma maandiko yanaelezea vizuri, Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” …Mtu anapoingia katika kitendo cha uzinzi maana yake anachafua HEKALU LA MUNGU..

sio hivyo tu hata kuchana chale ni kosa kubwa, Agano la kale liliwaamuru waIsraeli, “Msiikate miili yenu kwa ajili ya wafu wala kuchanja chale juu ya ngozi za miili yenu.Mimi ni Bwana” (mambo ya walawi 19:28)…Tambua matumizi ya MWILI WAKO….Heshimu mwili wako maana ni HEKALU TAKATIFU
Tunapaswa kufahamu kuwa miili yetu na nafsi zetu pia zimekombolewa na ni mali ya Mungu. Ijapokuwa haelekei moja kwa moja juu ya chale na alama za miili, 1 Wakorintho 6:19 -20 inatupatia kanuni moja, “Nini? Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mnaye kutoka kwa Mungu na ninyi si mali yenu wenyewe. Mmenunuliwa kwa thamani kwa hivyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambvyo ni vya Mungu.” Miili yetu sharti iandamane na ukweli kokote tuendako.
–Conrad Conwell.

Mwili wako ni wathamani

Vitu Vyote Vya THAMANI Hapa Duniani, Mungu Ameviweka Mahali Ambako Ili Kuvipata LAZIMA Ufanye Kazi Ya Ziada!
MAFUTA Ni Malighafi Ya Thamani Sana, Yako CHINI SANA Kuyapata Mpaka UCHIMBE CHINI SANA NA KWA GHARAMA... Ndivyo Ilivyo Kwa DHAHABU, ALMASI, TANZANITE Na Madini Yote Ya Thamani!

MWILI WA MWANAMKE Nao Ni KITU CHA THAMANI SANA, Kuliko MAFUTA, AU MADINI YOYOTE Unayoyafahamu Wewe... Ndio Maana Biblia Inasema SISI VIDUME TUKIPATA MKE TUMEPATA KITU CHEMA [Kwanza] LAKINI Pi...a TUNAKUWA TUMEPATA NA KIBALI CHA ZIADA TOKA KWA BWANA, Ambacho Kinakuja Tu UNAPOMPATA MWANAMKE Yaani "KITU CHA THAMANI"
(Soma Mithali 18:22 Ujiionee Hii Siri Ya Ajabu Sana)!

UKIMWONA MTOTO WA KIKE ANAACHA NJE KIUNGO CHOCHOTE CHA MWILI WAKE, Yawe MATITI, TUMBO, KITOVU, SEHEMU ZA MIGUU Nk, Wakati "VITU VIDOGO" KAMA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, MAFUTA Nk Vimefichwa Sana, USIMLAUMU, HUYO HAJUI THAMANI YAKE, HAJUI KUWA YEYE NI KITU CHEMA... HAJUI KUWA MWILI WAKE NI HAZINA YA PEKEE ANAYOPASWA KUISITIRI MPAKA ATAKAPOKUTANISHWA NA KUUNGANISHWA NA MMEWE AMBAYE KWA MUJIBU WA NENO LA MUNGU HUYO PEKEE NDIYE "MWENYE MAMLAKA JUU YA HUO MWILI"

ACHENI KUWAPA FAIDA WANAUME WENGINE, VIUNGO VYAKO MALI YA MMEO BWANA, MTUNZIE YEYE... Linda Heshima Na Utu Wako Eee Mwanamke Na Wewe Mdogo Wangu Uitwaye MSICHANA... Waache Wazungu WAMESHACHANGANYIKIWA NA MMOMONYOKO WA MAADILI WALIOSHINDWA KUUZUIA, WANATAKA KUTUSAMBAZIA SUMU NA SISI... Tushike Viwango Vya Neno La Mungu, Japo MAVAZI SI TIKETI YA KUKUPELEKA MBINGUNI!

Tusizidiwe AKILI Na Hawa Majirani Zetu Wana Wa Ishmaeli Wanaojisitiri Vema Maungo Yao... Ingawa Kweli Ndani Hawako Hivyo!

Wednesday, February 5, 2014

Vuka Historia Yako

Bwana YESU Asifiwe, kwanza nataka ujue kuna watu HISTORIA ya Maisha yao imesimama hapo hapo haiendi mbele wala hairudi Nyuma,Wakati Mwingine hali hii imesababisha hata watu wako wa karibu waone hiyo ni historia yako siku zote..Lakini nataka nikuambie HISTORIA HIYO leo inakwenda kubadilika,Watu wa karibu walimuona yule RAHABU kama ni kahaba aliyeshindikana na hata ndugu walikuwa wanamtegemea yeye na kazi ile ya Ukahaba,Ni kweli Rahabu alikuwa na msaada mkubwa sana kwa ndugu zake,lakini msaada ule ulikuwa na dosari (Shetani ndiye alikuwa anahusika) Rahabu alipochukua hatua ya kumsogelea MUNGU,MUNGU akambadilisha (Yoshua 6:25) “Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu,yule kahaba,na watu wa nyumba ya baba yake,na vitu vyote alivyokuwa navyo naye akakaa kati ya Israel hata leo;kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko”..
Ukiusoma huu mstari kwa umakini utaona Kupitia Rahabu nyumba nzima waliokoka, Biblia inatuambia akakaa kati ya Israel hata leo (Maana yake akahesabiwa ni kizazi cha Israel) Hujanielewa? Ebu soma hapa (Waebrani 11:31) “Kwa imani Rahabu,yule kahaba,hakuangamia pamoja na hao walioasi;kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani” Unaweza ukaona Rahabu alifanya kitu kidogo sana lakini kwa MUNGU ni kikubwa sana…MUNGU akaona vema Amuweke Rahabu katika kundi la wazee wa IMANI (Waebrania 11:39) “Na watu wote hao wakiisha kushuudiwa kwa sababu ya imani yao”
Ebu leo Vuka historia yako “Bwana yu pamoja nawe Ee shujaa (Waamuzi 6:12b) Vuka Historia yako leo,yawezekana una ugonjwa ambao waliumwa Babu/Bibi zako au Baba/Mama zako,yawezekana unahistoria ya kujikaata kuwa wewe haufahi au kuna dhambi umetenda unaona ni vigumu kurudi kwa MUNGU….Sikia nikwambie MUNGU anasamehe..Rudi leo….Rahabu aliporudi kwa MUNGU Historia MPYA ilifunguka katika maisha yake

MAMBO YA MSINGI 20 YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA HABARI YA DAUDI NA GOLIATHI 1SAMWELI 17:1-55, NA 18: 1-5.



                                                      
1.JINA LA YESU lina uwezo mkubwa kuliko majina yote. Daudi akasema nakujia kwa Jina la BWANA. Tumia jina hilo unapotaka maombi yako yawe na ushindi. 

2.Mawe matano yanawakilisha huduma tano, uchungaji, utume, unabii, ualimu na uinjilisti. Hawa wote wanatakiwa kuwepo katika kanisa na kulelewa namchungaji ndio maana ya Daudi kuweka mawe hayo ndani ya mkoba wa kichungaji.

3.Daudi alichukua mawe matano pia kwa sababu alipeleleza na kujua Goliathi ana ndugu wengine wanne wenye mwonekano kama wake (THEOLOGY). Katika hili tunajifunza kujipanga kwa changamoto za baadaye hata kama bado hazijafika. Kama leo ni shwari basi jipange kwa ajili ya Kesho. Kwa lugha ya uchumi tunasema jifunze kuweka akiba.

4.Upako wa Kwanza ulimpa Daudi nguvu ya kujihesabia mshindi hata kabla ya watu kujua kuwa yeye ni mshindi. Alitafuta kutumia nguvu yake. Usikae kimya wakati kuna jambo linaharibika na unajua kabisa unao uwezo wa kuweka mambo kwenye mstari.

5.Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Sauli na majeshi ya Israeli walijiona wanyonge na dhaifu kwa Goliathi.(walifadhaika na kuogopa sana) lakini Daudi alijiona kuwa mshindi na kweli akamshinda Goliathi.

6.Daudi alitumia silaha dhaifu (kombea na jiwe) lakini alishinda, maana yake hata kama unahisi huna nguvu nyingi, huna pesa nyingi, huna jina kubwa, huna elimu kubwa, unadharaulika kama Goliathi alivyomdharau Daudi, Mungu akikutia nguvu, kile kidogo ulichonacho kinaweza fanya mambo makubwa saana! Efeso 3:20 Mungu hufanya zaidi hata tuwazayo na tuombayo.

7.Daudi hakutafuta umaarufu, kwa sababu kama angependa umaarufu basi baada ya kuua dubu na simba angejitangaza lakini alitulia mpaka alipokutana na Goliathi. Tena hata baada ya kumuua Goliathi ni wana wa Israel walioanza kumwimbia nyimbo nzuri zaidi ya zile za mfalme. Si yeye aliyejitangaza. Nia yake haikuwa kujulikana bali kufanya mapenzi ya Mungu. Usihubiri au kuimba ili tukujue bali fanya kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu. Mungu akikuinua hutapata shida ya kujitangaza.

8.Mungu huwainua watu kutoka kiwango kimoja kwenda kingine. Upako mmoja hadi mwingine. Daudi alipomuua simba na dubu ndipo alipoweza kumuua Goliathi. Unapotulia na kunyenyekea chini ya Mkono ulio hodari wa Mungu,basi Yeye atakuinua kwa wakati wake(1Petro 5:6). Muda mwingine Mungu anaonekana kama anachelewa kwa sababu tunataka kuruka hatua, katika maisha yako, Mungu anajua hatua unazotakiwa kupita, ukiisha kuua simba na Dubu Mungu atakuwezesha kumuua Goliathi. Mungu anapotaka kukuinua lazima aruhusu tatizo ambalo wewe peke yako ndo utakuwa na jibu lake.

9.Tunajifunza pia kwamba matatizo siku zote yapo tu haijalishi unafanya kazi gani. Usifikirie kwamba ukiwa mtumishi basi majaribu yanapungua.ooh, mengi tu. Popote ulipo jifunze kuwa mwaminifu na Bwana atakuinua. Daudi alikuwa mwaminifu kwa kuhakikisha usalama wa wanyama malishoni ndipo Mungu akamwamini na kumpa Taifa zima la Israel. Umeshindwa kuongoza familia yako, utawezaje kuendesha kanisa la watu mia? Umeshindwa kuongoza idara ya watu 6 unataka kuwa mkurugenzi wa kampuni ili iweje? Usije sema labda nikioa ndo nitaacha uzinzi, labda nikipata milioni mia ndio nitaacha wizi, au labda nikibadilishiwa kazi ndo nitaacha rushwa. HAPANA, tenda kwa uaminifu hapohapo ulipo na Bwana atakuona.

10.Katika kila jambo, hata kama dunia nzima watasema hili haliwezekani wewe soma LUKA 1:37. “hakuna la kumshinda Mungu” Ndio maana kaka zake walipomkebehi Daudi, yeye hakujali akamfuata Goliathi na kumuua. Vikwazo vya mafanikio yako vinaweza kutokea hata ndani ya familia yako au kwa watu wako wa karibu sana, tena wanaoonekana wenye uwezo kuliko wewe, hakuna sababu ya kukata tamaa ni mwanzo mwisho tunasonga mbele. Umetengwa baada ya kumpokea Yesu? Kaza buti songa mbele mpaka Goliathi atie amri chini.

11.Daudi hakufurahia watu wa Mungu wanapotukanwa. Kama mtu wa Mungu kamwe usifurahie watu wanapomsema mtumishi wa Mungu vibaya, hata kama ni kweli katenda uovu, endapo ni mpakwa mafuta wa Bwana kuna utaratibu wa kuyasema na si kuropoka tu. Kumbuka watu wa karibu ya Musa waliadhibiwa na Mungu kwa sababu walimsema vibaya Musa japokuwa ni kweli alikosea.

12.Vita kati ya wana wa Israeli na wafilisti vinawakilisha vita vya watu wa Mungu dhidi ya Shetani na jeshi lake na imetupasa kulishinda kwa kukaa ndani ya Neno(ujumla wa huduma tano kanisani) na kulitumia Jina la Bwana.

13.Shetani ana mikwara mingi sana. Anatumia ufahamu wetu kutufanya tuhisi kwamba yeye anaweza zaidi yetu. Goliathi alitumia muda mwingi kuwatisha majeshi ya wana wa Israeli, kama ilivyo leo shetani anavyokutisha kwamba hutapona, hutafanikiwa, utakufa, utachekwa ukiokoka nk. Daudi hakutishwa kamwe. Unapoiruhusu roho ya hofu ndani yako basi unafanyika mateka wa Shetani. Tunatakiwa kuangusha ngome za fikra zetu zipate kutii uwezo wa Jina la Bwana badala ya kuogopeshwa na matatizo. Tatizo lako ni la muda mfupi tu amini sasa na Bwana atakutokea na kukushindia.

14.Usijadiliane na adui. Wana wa Israeli walitakiwa kujipanga kuvamia, kwa mfano wangeamua watu sita wamvamie Goliathi na wengine wavamie jeshi la wafilisti wangemaliza kelele zote za Goliathi. Kitendo cha kujadiliana na Goliathi kilimpa Goliathi nafasi ya kuingiza hofu mioyoni mwao, don’t compromise with devil’s deceptions /techniques.

15.Daudi alivaa nguo za kijeshi lakini akavua baada ya kuona hazimfai. Maana yake unaweza kujaribu suluhisho/njia za mtu mwingine lakini haishauriwi kwa sababu Mungu alikuumba wewe original, unapocopy na kupaste maana yake uwezo wako na wajibu wako unauweka kuwa kipolo na ufanisi wako unaweza kuwa na matunda kidogo. Japokuwa unaweza usijue kama matunda yako ni madogo. Usiseme kwa sababu wengi wanasoma sheria au udaktari basi na mimi lazima nisome, usiseme kwa kuwa wengi wanapinga Injili basi na mi naogopa kuwa wa tofauti. Mungu alikuumba ukiwa tofauti kabisa na watu wengine, Mungu huwa hafanyi duplications. Anaumba vitu vipya. Hata mapacha wa kufanana nao wanatofauti kubwa sana. Mungu ana kusudi na maisha yako, tafuta kujua na utende vema.

16.Kuwa na umri mdogo si kigezo cha kukuzuia kufanya mambo makubwa ya ufalme wa Mungu. Daudi alikuwa na miaka 17 wakati anamuua Goliathi. Alikuwa mtoto wa mwisho na aliyedharaulika (katika sura ya 16 mzee Yese hakumuhesabu kati ya watoto wake lakini Samweli alisisitiza kama yuko mwingine ndipo Yese alipoagiza Daudi aitwe kutoka malishoni) lakini alitoa suluhisho la nchi nzima. Jitambue na kuelewa ni hazina gani Mungu ameweka ndani yako! Leo kuna milionea wengi tu ulaya ambao wana umri wa miaka ishirini, hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao. Hii ndio sababu sioni ugumu kufundisha na kuandika masomo ya mahusiano, kwa sababu Mungu amenifundisha hata kabla sijaoa.

17.Mtu asiyetahiriwa (asiye na agano la Mungu, yaani mganga wa kienyeji, mchawi, mshirikina, kibaka, mwuaji, na wafananao na hao) hana uwezo wa kuyatisha maisha yako ukimtegemea Kristo.

18.Daudi akasema asizimie moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu, mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na mfilisti huyu. Nami nakuambia leo usizimie moyo kwa ajili ya jambo hilo (Ukosefu wa ajira, ugonjwa, fitina, umasikini nk) maana katika yote tunaye atushindiaye, Kristo atayamulika mapito yako na kukushika kwa mkono wake wa kuume pale tu utakapoamua kumwamini kwa moyo wako wote.

19.Daudi alimkata kichwa Goliathi kwa upanga (Neno la Mungu ni kama upanga). Kwa hiyo hakikisha unapoingia vitani una neno la Mungu la kutosha na unaliweka katika matendo, hata Yesu alipojaribiwa alitumia Neno la Mungu kwa ufasaha na akamshinda shetani.

20.Mfalme Sauli hakumwacha Daudi arudi nyumbani kwake. Unapokuwa mshindi, yaani umeleta suluhisho au kufanya jambo la kipekee sehemu fulan(kanisani, ofisini, idarani, wizarani, ndani ya taasisi nk) lazima heshima yako itapanda tu, bosi atatamani uwe assistant wake, Daudi kutoka malishoni mpaka kuishi ikulu si mchezo. Fanya vizuri sehemu uliyopo ndipo Mungu atakupeleka hatua ya juu zaidi, kuwa mnyenyekevu, mwenye bidii na mcha Mungu. 


BARAKA ZA BWANA

Mwana Kondoo
  "Baraka za Mungu zinapokuja kwa mtu humbadilisha mpaka jina.
Kabla ya baraka aliitwa YAKOBO baada ya baraka akaitwa ISRAEL .Kabla ya baraka aliitwa ABRAHAM Baada ya baraka akaitwa IBRAHIM,
Kabla ya baraka unaitwa MASIKINI ukibaliwa utaitwa TAJIRI.Ombi langu Mungu akupe jina jipya ktk jina la YESU.