Thursday, February 5, 2015

SABABU SABA (7) ZITAKAZO KUFANYA KUWA MSHINDI DUNIANI...

Glory to GOD watu wa MUNGU,leo ninataka nizungumze na wewe Sababu saba zitakazokufanya kuwa Mshindi Duniani...Zifuatazo ni Sababu hizo..
1.NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO..
Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi lakini ndano yako kukiwa na Maneno mengine kinyume na Neno la MUNGU unaweza ukatikiswa na adui na kujikuta umeanguka.ndio Maana Mfalme Daudi akasema "Moyoni Mwangu nimeliweka Nno lako nisikutende dhambi" Zaburi 119:11,Je moyoni mwako wewe umeweka neon la namna gani??
2.MAOMBI/KUOMBA....
Daniel,Eliya,Mussa,Bwana YESU,nk Hawa wote walihakikisha wanaishi katika Maombi,Wakati Mwingine kwa kufunga,Bwana Yesu kuna sehemu aliwaambia wanafunzi wake hamkuweza kukesha name hata saa moja
Matayo 26:40 Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, "Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu."
3.MAONO..
Hakikisha katika maisha yako Duniani unakuwa na maono,(Yaani mtazamo wa Mbeleni) hata kama wenzako hawajafika wewe unasema nitafika,usiishi bila maono,ukiwa na maono mipango yako inakuwa inaenda vizuri pasipo na shida.
Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi kuchukuliwa na upepo na kupelekwa usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa ujumla.
Mithali 29: 18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
4.KUTOKUWA NA TAMAA YA VITU VISIVYOFAA
Kuna watu wanatamani vitu visivyofaa ambavyo ni kinyume na agizo la MUNGU,Ndiyo maana MUNGU hakasema usitamani mke wa jirani yako,wengine wanatamani mali za wengine bila kujua chanzo chake na wengi wamepotea kwa namna hiyo
Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.
5.AMBATANA NA MARAFIKI WEMA..
(Mithali 27:17) Chuma hunoa chuma. ni dhahili chuma hakiwezi kunoa embe angalia marafiki zako wanakunoa au?? angalia mtazamo wao,kuwaza kwao,nk..Wao waliokutana na Marafiki wabaya,ambao wamesababisha mpaka maono yao kufa na kurudi nyuma kwa kumuacha YESU KRISTO..Wapo waliokutana na marafiki wabaya waliokuwa na lugha chafu na kusabadilisha..Je una marafiki wa aina gani??
6.KUTOMWEKEA MUNGU MIPAKA
Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi...kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni 'DHARAU' kwake... Zaburi 78:41 inasema, "Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel"Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya 'Maziwa na Asali'...10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki...majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema...waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni 'UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO' wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi...WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO...Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako...ishi maisha ya IMANI...Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, "Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia" Isaya 55:8-11
7.KUACHA DHAMBI
Dhambi ni mbaya...inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako...inakufanya ufe kabla ya muda wako...Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako...unafanya kazi ambayo mshahara uitwao 'MAUTI' utaupata.Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, "Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" pia Biblia inasema, "Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa"Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi...Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!
Mwl.Conrad..
0753 391634