Saturday, March 21, 2015

KWELI KUHUSU PASAKA!

HALELUYA WAPENDWA... NATAMANI KWA POSTI TUUFUHAMU UKWELI,HULAZIMISHWI KUAMINI,LAKINI UKIELEWA INATOSHA.
NENO PASAKA LIMETOOLEWA TOKA KTK MATAMSHI YA KIEBRANIA PESACH/PASAKH AU PASSOVER KWA KIINGEREZA,LIKIWA NA MAANA YA "PITA JUU YA" LINATAJWA KWA MARA YA KWANZA KTK KUTOKA 12:11 ;
WAYAHUDI WALIELEKEZWA KUPAKA DAMU YA KONDOO AU MBUZI(KUTOKA 12:5) KATIKA MIIMO YA MILANGO,ILI YULE MALAIKA MHARABU(DESTROYER) ATAKAPOPITA JUU YA MISRI AKIIONA DAMU KTK "DOOR POSTS" AKAWA ANAPASAKA(PITA JUU) ASIPOIONA DAMU ANAUA WAZALIWA WA KWANZA. MUNGU AKATOA MAELEKEZO HIYO SIKU WAISHEREKEE KAMA AMRI YA MILELE(KUTOKA 12:14) SASA NAMNA YOTE YA KUIADHIMISHA PASAKA KWA KIYAHUDI,TARATIBU ZIPO KTK SURA HIYO YOTE YA 12. MTUME PAULO KWA UFUNUO ANAMFANANISHA YESU NA YULE MWANAKONDOO WA PASAKA,NAYE AMECHINJWA KWA UKOMBOZI WETU,NAAM YEYE NDIYE PASAKA WETU (1KOR 5:7-8) .
MUHIMU:
UKRISTO SIO DINI YA KIYAHUDI(JUDAISM) INGAWA ILIANZA KAMA SECT(DHEHEBU) NDANI JUDAISM
JE!PASAKA NI EASTER?
KOSA KUBWA SANA NI WATU KOKOSA MAARIFA NA KUSEMA TUNASHEREHEKEA EASTER,EASTER SIO PASAKA NENO EASTER NI LA KIINGEREZA LIMETOKANA NA JINA "ISTHAR" THE BABYLONIAN GOD OF FERTILITY ,MUNGU WA UZAZI WA BABELI,NDIO MAANA MAPAMBO YA EASTER HUKO ULAYA NI MAYAI EITHER PICHA AU VITU VILIVYOTENGENEZWA KWA PLASTICS AU RUBBER. JARIBU KWENDA GOOGLE-IMAGES TAFUTA "EASTER ORNAMENTS" UTALETEWA MAPAMBO YA EASTER NI MAYAI. SASA MAYAI HAYANA UHUSIANO NA IMANI YA UKRISTO,MAYAI YAMETAJWA KTK BIBLIA,LAKINI OCCASIONS MBILI TUU ZA MAANA NA SIO KWAMBA YAMEHUSIANISHWA NA IMANI. MABISHOPS WA KARNE YA TATU WALIPOONA KUNA SHEREHE ZA KIPAGANI WAKAONA NI HERI HIZO TAREHE WAACHANE NA ULE UPAGANI WAAZIMISHE MATUKIO MUHIMU YA UKRISTO,IKUMBUKWE HAKUNA KALENDA YA KIKRISTO,THE GREGORIAN CALENDER REPLACED THE JULIAN CALENDAR NA NDIYO ITUMIKAYO DUNIANI KOTE,HATA WALE WENYE KALENDA ZAO ZA KIDINI WANAITUMIA HII PIA.NITAFAFANUA CHINI KIDOGO
INASHEREHEKEWAJE SASA?
PASAKA YA WAYAHUDI NI TAREHE 14 MWEZI NISANI,IKUMBUKWE KALENDA YA WAYAHUDI MUNGU ALIIFANYIA AMENDMENT WAKATI ANAWATOA MISRI (KUTOKA 12:2) ALIWAAMBIA HUU UTAKUWA MWANZO WA MIEZI KWENU,
KUMEKUWA NA HOJA AMBAZO NI MATOKEO YA KUTOELEWA MAMBO.
HEBREW CALENDAR NA SECULAR CALENDAR HAZIFANANI KWA LOLOTE!
THE TIME WATU WATACHANGANYIKIWA NI PALE MNAPOTAKA KUITAJA UKIWA UNATUMIA HII GREGORIAN CALENDAR!
ANAYETAKA KUELEWA ASOME HAPA
WIKI ILIYOISHA TAREHE 15 (INGAWA JUMAPILI NI SIKU YA KWANZA YA JUMA NAIWEKA HIVI NISICHANGANYE WAZO JINGINE),ILIANZA TAREHE 9
YAANI 9 MARCH 2015 TAREHE HIYO KWENYE CALENDAR YA KIYAHUDI ILIKUWA TAREHE 27 ADAR 5773 ,SASA HUO MWEZI WAO ADAR NI WA MWISHO KTK KUHESABU TOKA MWEZI NISANI. MWEZI NISANI WA KIYAHUDI NI WA KWANZA,LAKINI KWENYE SECULAR CALENDAR,TOFAUTI YA MIEZI MITATU ILITOKANA NA MUNGU KUWAAMBIA WAISRAEL "HUU UTAKUWA MWANZO WA MIEZI KWENU" WAKATI ILIKUWA MWEZI WA ABIBU(YAANI WA TISA)
SASA WANAOTAJA 14 NISANI KUWA NI PASAKA,HAPO SIO JANUARY,MNAPASWA KUONGEZA MIEZI MITATU ILI KU-MATCH NA CALENDAR ZENU MLIZOBANDIKA SITTING ROOMS,WALE BISHOPS WALIO ''SWAP'' ILI KUONDOA SIKUKUU ZA KIPAGANI,WALIZINGATIA HILONDICHO WALICHOFANYA MWAKA 368A.D KUHUSU 25 DESEMBA YAANI KRISMASI,MAADHIMISHO YA ISTHAR FELL IN THE MID APRIL,INGAWA INATOFAUTIANI NA HATA KUANGUKIA MARCH MWISHONI. KILICHOLENGWA NI YALE MAJIRA.MNAWEZA KUCHANGANYIKIWA MTAKAPOKUTA CALENDAR YA KIYAHUDI WAMEIMECHISHA NA SECULAR LAKINI YAO MWEZI HUU HATA TAREHE 30 HAIPO,MNAWEZA KUIDOWNLOAD TU GOOGLE STORE..
JE NI UPAGANI KUSHEREHEKEA/KUADHIMISHA PASAKA?
NDUGU WAPENDWA WAPO WANAONA SI VYEMA,NA WAPO WANAONA NI VYEMA ULIMWENGU UKUMBUSHWE KILA MWAKA KUWA YESU ALIZALIWA,ALIKUFA KWA MAUTI YA MSALABA NA KUFUFUKA,HAKUNA HAJA UGOMVI WALA KUHUKUMIANA,ANAYEONA HAIFAI AACHE,NA WANAOONA VYEMA WAADHIMISHE.HAKUNA UPAGANI MAANA KTK SECULAR KALENDA EASTER NI SEASONS NA SIO KUMWABUDU MUNGU WA UZAZI WA BABELI,NDIO MAANA WAKRISTO KWA MAJIRA HAYO HATUPAMBI MAYAI,WALA HATUFANYI LOLOTE LILILOKUWA LIKIFANYWA NA WALE WAPAGANI,BALI TUNAITANGAZA KWA WAZI MAUTI NA KUFUFUKA KWA YESU,TUKIJIDHILI KWA KUFUNGA NA KUOMBA MAJIRA HAYA YA PASAKA. KUNA WANAOSEMA PASAKA NI MEZA YA BWANA,HIZI NI DOCTRINES TOFAUTI ZA MADHEHEBU HATUWEZI FANYA WABADILISHE .
MFANO MEZA YA BWANA MITUME NA WAKRISTO WA KWANZA WALIIFANYA REGULARLY KILA WALIPOKUTANA,NA JE NDIVYO INAVYOFANYWA KTK MADHEHEBU YOTE?KILA MKIKUTANA MNASHIRIKI MEZA YA BWANA?NA KAMA NDIVYO MBONA INATOFAUTIANA NA MAANA ILE YA PASAKA YA TAREHE 14NISANI,AMBAYO INAANGUKIA TAREHE FULANI ZA MWEZI WA NNE?NA HAYA MAANDIKO MATH 26:1-2,MARKO 14:1,LUKA 2:41-41,YANAONESHA MAJIRA YA PASAKA YA KIYAHUDI NDIYO MAJIRA YA PASAKA YA KIKRISTO,YESU ALIPOKUJA ALISHIRIKI YOTE KWA TARATIBU ZA KIYAHUDI SIO ZA KIKIRISTO,AMBAPO UKRISTO ULIKUJA KUWA DINI KAMILI HUKO MBELE YESU AKIWA AMEONDOKA KITAMBO.WAFUASI WA YESU WALIITWA WANAFUNZI WA YESU,BADAE WAKRISTO(MDO 11:26)
IKUMBUKWE:
CHRISTIANITY IS NOT THE JEWISH RELIGION THOUGH IT BEGAN AS THE SECT WITHIN JUDAISM.
WANAOTAJA TAREHE 14NISANI HIYO NI TAREHE NGAPI KWA KALENDA TUNAYOITUMIA?...
TOFAUTI YA MIAKA
TANGU AZALIWE YESU MWAKA (4BC) LEO NI MWAKA 2015,LAKINI HUU NI MWAKA WA 5773 KWA WAYAHUDI,NA NI MWAKA WA 1436 KWA WAISLAMU.
IT IS THE CONTENT THAT COUNTS!

mwl.proo 0762879363

Thursday, March 19, 2015

POMBE NI HATARI KATIKA SAFARI YA KWENDA MBINGUNI

1 timotheo 5:23
Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo Mara kwa Mara.
QN ...
A. Mvinyo uliotajwa hapo ni pombe

B. Kwann Paul alimwambia timotheo atumie mvinyo ili apone kwann hakumwombea kwa Mungu ili amponye
KUNYWA POMBE NI DHAMBI KWA WATU MUNGU,HAKUNA UTETEZI WOWOTE WA KIBIBLIA. JAMBO LA KWANZA LUGHA YA KISWAHILI HAIKUWA NA MANENO YA KUTOSHA KUTAJA AINA ZOTE ZA DIVAI/MVINYO/VILEO. KTK ULIMWENGU WA ULE WA ZAMA ZA BIBLIA HUSUSANI UYAHUDI NA UYUNANI,WALIKUWA NA MANENO TOFAUTI KUTOFAUTISHA KINYWAJI HUSUKIA TOKA KWENYE ZAO LA ZABIBU. NI KAMA AMBAVYO CRUDE OIL IKIPITIA REFINING PROCESS HUTOA PETROL,DIESEL,KEROSENE ETC VIVYO HIVYO ZAO LA ZABIBU HUTOA DIVAI KILEO,DIVAI PURE JUICE,DIVAI DAWA ,ZABIBU KAVU ETC
HAYA NI MAJINA YANAYOTOFAUTISHA AINA HIZO KAMA YANAVYOONEKANA KWENYE HEBREW BIBLE(TANAKH) NA GREEK BIBLE(SEPTUAGINT)
(1)TYROSH PURE JUICE OF CANA (JOHN 2)
(2.) YAYIN THE MOST COMMON WINE IN THE BIBLE
(3)CHEKAR
(4.)MAMCHAK
(5.)GATH
KATIKA HIZI ZIPO AMBAZO NI DAWA ZA KUPAKA VIDONDA TUYATAZAME HAYA MAANDIKO FROM OJB
PROV 31:6
|6| Give strong drink unto him that is ready to perish, and yayin unto those that be of bitter nefesh.
JH 2:10
|10| And the Rosh HaMesibba says to him, Everyone sets out the yayin hatov first, and when they have become drunk, he sets out the inferior; you have kept the yayin hatov until now. |11| This was the reshit
1TIM 5:23
|23| No longer drink only mayim, but use a little yayin because of your stomach and your frequent illnesses.
DIVAI ILIYOKUWA NI JUICE PURE NA HALALI KUNYWEWA BILA SHARTI NI TYROSH,INGAWA YAYIN NDIYO ILIKUWA THE MOST COMMON DIVAI. SASA HATUNA BUDI KUJUI DIVAI WAS A CUSTOMARY ACCEPTED DRINK,INGAWA TUNAKUMBUKA MUNGU ALIWAKINGA WATU KADHAA WALE ALIOWATENGA KWA KUSUDI LAKE,MAKUHANI ETC,BILA SHAKA UNAKUMBUKA MKE WA MANOA AND ALL SUIT-STORIES.
SASA LET ME CLEAR A DOUBT ON TIMOTHY. HUYU MCHUNGAJI TIMOTHEO ALIISHI KTK MJI WA EFESO,THE WATER OF THE CITY YALKUWA SALTY AND HARD.WENGI HAWAKUWA WANAPENDELEA KUNYWA MAJI AKIWEMO TIMOTHEO,SASA KWA KUWA WATU WALIKAA HATA JUMA ZIMA BILA KUNYWA MAJI,WENGI WALIPATA SHIDA YA MATUMBO KTK MMENG'ENYO (CONSTIPATION),TIMOTHEO SUFFERD THE SAME,SASA PAULO ALIKUWA ANASHAURI "WATER THERAPY" ,AMBAPO WATU WALICHUKUA MAJI NA KUYACHANGANYA NA YAYINI KIDOGO ILI YAWE NA TASTE UWEZE KUNYWA. THE REASON BEHIND WAS NOT ULEVI,INGAWA BADO MSIMAMO WA MWISHO KUHUSU KILEVI NI "USIGUSE,USISHIKE,USIONJE" KOLOSAI 2:21
TUTAKUWA WAJINGA KAMA TUTALAZIMISHA UKRISTO WETU TUUFANANISHE NA ULIMWENGU WA KALE WA UJINGA (MATENDO 17:30) AMBAPO MUNGU HAKUWA AMEJIFUNUA KWA UKAMILIFU,WE ARE LIVING AT THE MAXIMUM REVELATION ERA
🍷gonga tuu kama hupendi mbingu

Thursday, February 5, 2015

SABABU SABA (7) ZITAKAZO KUFANYA KUWA MSHINDI DUNIANI...

Glory to GOD watu wa MUNGU,leo ninataka nizungumze na wewe Sababu saba zitakazokufanya kuwa Mshindi Duniani...Zifuatazo ni Sababu hizo..
1.NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO..
Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi lakini ndano yako kukiwa na Maneno mengine kinyume na Neno la MUNGU unaweza ukatikiswa na adui na kujikuta umeanguka.ndio Maana Mfalme Daudi akasema "Moyoni Mwangu nimeliweka Nno lako nisikutende dhambi" Zaburi 119:11,Je moyoni mwako wewe umeweka neon la namna gani??
2.MAOMBI/KUOMBA....
Daniel,Eliya,Mussa,Bwana YESU,nk Hawa wote walihakikisha wanaishi katika Maombi,Wakati Mwingine kwa kufunga,Bwana Yesu kuna sehemu aliwaambia wanafunzi wake hamkuweza kukesha name hata saa moja
Matayo 26:40 Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, "Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu."
3.MAONO..
Hakikisha katika maisha yako Duniani unakuwa na maono,(Yaani mtazamo wa Mbeleni) hata kama wenzako hawajafika wewe unasema nitafika,usiishi bila maono,ukiwa na maono mipango yako inakuwa inaenda vizuri pasipo na shida.
Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi kuchukuliwa na upepo na kupelekwa usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa ujumla.
Mithali 29: 18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
4.KUTOKUWA NA TAMAA YA VITU VISIVYOFAA
Kuna watu wanatamani vitu visivyofaa ambavyo ni kinyume na agizo la MUNGU,Ndiyo maana MUNGU hakasema usitamani mke wa jirani yako,wengine wanatamani mali za wengine bila kujua chanzo chake na wengi wamepotea kwa namna hiyo
Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.
5.AMBATANA NA MARAFIKI WEMA..
(Mithali 27:17) Chuma hunoa chuma. ni dhahili chuma hakiwezi kunoa embe angalia marafiki zako wanakunoa au?? angalia mtazamo wao,kuwaza kwao,nk..Wao waliokutana na Marafiki wabaya,ambao wamesababisha mpaka maono yao kufa na kurudi nyuma kwa kumuacha YESU KRISTO..Wapo waliokutana na marafiki wabaya waliokuwa na lugha chafu na kusabadilisha..Je una marafiki wa aina gani??
6.KUTOMWEKEA MUNGU MIPAKA
Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi...kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni 'DHARAU' kwake... Zaburi 78:41 inasema, "Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel"Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya 'Maziwa na Asali'...10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki...majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema...waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni 'UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO' wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi...WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO...Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako...ishi maisha ya IMANI...Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, "Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia" Isaya 55:8-11
7.KUACHA DHAMBI
Dhambi ni mbaya...inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako...inakufanya ufe kabla ya muda wako...Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako...unafanya kazi ambayo mshahara uitwao 'MAUTI' utaupata.Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, "Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" pia Biblia inasema, "Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa"Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi...Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!
Mwl.Conrad..
0753 391634

Monday, January 12, 2015

MAJINA YA MUNGU



Jina la Mungu Maana yake Mstari wa Biblia
...
1. Adonai ‐ Mungu Mwenye enzi yote ‐ Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐32. El‐Ohim ‐ Mungu Muumbaji ‐ Mwa 33:20, Kol 1:16‐17
3. El‐Elyon ‐ Mungu Aliye juu zaidi ‐ Mwa14:18, Dan 4:34
4. El‐Gibbor ‐ Mungu Mwenye Nguvu ‐ Isa 9:6, Zab 147:5
5. El‐Hai ‐ Mungu Aliye Hai/Anaishi ‐ Josh 3:10, 1Sam17:26
6. El‐Olam ‐ Mungu wa Milele ‐ Ufu 4:8, Kut 3:14
7. El‐Roi ‐ Mungu Aonaye kila kitu ‐ Mith 15:3, Zab 32:8
8. El‐Shaddai ‐ Mungu Mtoshelezi ‐ Mdo 17:28, Kumb 8:4
9. Jehovah ‐ Ajitegemeaye kuwepo ‐Kut 6:2‐8, Mdo 17:24‐25
10. Jehovah Shalom ‐Mungu Amani yetu ‐ Amu 6:22‐24
11. Jehovah Rapha ‐ Mungu Atuponyaye ‐ Kut 15:26
12. Jehovah Jireh ‐ Mungu Mtoaji wetu ‐ Mwa 22: 8, 14
13. Jehovah Nissi ‐ Mungu Ushindi wetu ‐ Kut 14:13‐14
14. Jehovah Saboath ‐ Bwana wa Majeshi ‐ Malaki 3:7
15. Jehovah Shammah ‐ Bwana ni Aliyepo ‐ Kut 3:14
16. Jehovah Rohi ‐ Bwana ni Mchungaji wangu ‐ Zab 23:1
17. Jehovah Tsidkenu ‐ Bwana ni Haki yetu ‐ Yer 23:6
18. Jehovah Mekaddishem ‐ Bwana Atutakasaye ‐ Kut 31:13

Saturday, December 20, 2014

UBATIZO KAMA UNAVYOFUNDISHWA NA BIBILIA.

 
 
UBATIZO KAMA UNAVYOFUNDISHWA NA BIBILIA.
Nimeona ni vema nichukue muda wangu kidogo kuandika juu ya somo hili nyeti ambalo limekuwa sababu ya mvutano mkubwa sana katika mwili wa Yesu Kristo hususa katika nchi yetu.
Binafsi ninapozungumzia mwili wa Yesu Kristo nazungumzia kila mmoja ambaye amesafishwa na damu ya Yesu Kristo na kufanya uamuzi wa kumpa Yesu maisha yake kwa njia ya kuokoka. Mwili wa Yesu Kristo haujumuishwi na madhehebu ya Kikristo yaliyopo bali na watu toka madhehebu hayo yote ambao wameoshwa dhambi zao kwa damu ya Yesu baada ya kufanya maamuzi ya kumpa Yesu maisha yao, yaani wameokoka au wamezaliwa mara ya pili. Mwongozo thabiti wa watu hawa sio misimamo ya madhehebu wanayotoka bali ni neno la Mungu na ndicho kinachotuunganisha wanamwili wa Kristo bila kujali tumetoka madhehebu gani. Kwa kuwa kila dhehebu, kanisa na huduma lina utaratibu wake wenyewe kiunganishi kikuu cha watu wa Mungu toka madhehebu haya ni neno la Mungu ambalo pia linajulikana kama Bibilia au Maandiko Matakatifu.
Sasa ni dhahiri nikisema hivyo kwamba kila kanisa, huduma na dhehebu, lina utaratibu wake wa kubatiza. Wengine wana batiza watoto, wengie kwa maji machache, wengine kwa maji mengi nk. Nia ya fundisho hili sio kuingilia taratibu za makanisa, huduma au madhehebu za kubatiza bali ni kuleta ufahamu juu ya ubatizo ambao Yesu aliuagiza ambao huo hauna uhusiano hata kidogo na batizo zingine za kimapokeo ambazo zinaendelea katika makanisa, madhehebu au huduma mbalimbali.
Kila ubatizo upo kwa sababu zake na kwa makusudi yake. Ni wajibu wangu katika somo hili kufundisha ule ambao uliagizwa na Yesu.
UBATIZO NI NINI?
Neno ubatizo kama linavyotumika katika maandiko ya Agano Jipya linamaanisha kuzamisha ndani ya, linamaanisha kuzika katika, linamaanisha kufunika kabisa na.
Tukianzia kwenye maana ya neno ubatizo na jinsi ambavyo limetumika katika bibilia hakuna kiashiria chochote kwamba hili zoezi linaweza likafanywa kwa kunyunyiza au kuogesha na maji. Ni wazi tukianzia kwenye maana hili zoezi katika utekelezaji wake litahitaji tu maji mengi ili kulikamilisha. Kwa hiyo ubatizo ni wa maji mengi na mhusika lazima azamishwe kabisa ndani ya maji hayo, afunikwe kabisa na hayo maji na azikwe kabisa ndani ya hayo maji.
Tunavyoendelea kutafakari hili somo kimaandiko tutazidi kuona kweli hii ikijidhihirisha tena na tena na tena katika maandiko na tutaona kabisa kuwa ubatizo aliyouagiza Yesu ni wa maji tele na huu hauna uhusiano kabisa na batizo za kimapokeo ambazo baadhi ya makanisa na madhehebu ya Kikristo wanatumia kuwathibitisha waumini wao.
Hii itatusaidia kama mwili wa Kristo kujua kuwa tukishamwamini Bwana Yesu na kuamua kuokoka inatupasa kubatizwa kwa ubatizo huu aliyouagiza hata kama awali kabla ya kuamini tulibatizwa katika madhehebu yetu, maana ule ubatizo tuliyobatizwa katika madhehebu yetu kabla ya kumwamini Yesu na kumfanya Bwana na Mwokozi wa Maisha Yetu una maana yake na huu aliyoagiza Yesu nao una maana na umuhimu wake.
MAANDIKO YANAFUNDISHA NINI KUHUSU UBATIZO?
Tuanze mjadala katika kipengele hiki kwa andiko la muhimu sana katika kuuanzisha mjadala huu na somo hili.
Waebrania 6: 1 - 3.
Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Na hayo tutafanya Mungu akitujalia. (EBR. 6:1-3 SUV).
Kwa mujibu wa hili andiko ubatizo miongoni mwa mafundisho mengine ni fundisho la kwanza au la msingi katika Ukristo. Msingi ni wa muhimu sana na ndiyo unaobeba jengo zima. Msingi ukiwekwa vibaya jengo linalokuja kujengwa juu yake hautakuwa na uhakika wa uimara.
Kwa kuwa ubatizo ni somo la msingi kulipuuzia na kulifanya halina umuhimu ni kosa kubwa sana kwa mujibu wa hili andiko. Kusema kuwa ukibatizwa na maji mengi au machache yote yatakauka ni kudharau mafundisho na maagizo ya Yesu juu ya hili na ni kupuuza na kubeza agizo la muhimu sana ambalo lilitolewa na Yesu Kristo. Umuhimu wa ubatizo sio kama unakauka au hukauki ni nani aliagiza ifanyike na iliagizwa ifanyike kwa utaratibu gani?
Kwa kuwa ubatizo ni moja ya maagizo ya msingi ya Yesu Kristo kwa kanisa kama tukipuuza hili agizo tutakuwa tumepuuza kitu cha muhimu sana ambacho kitasababisha msingi wa maisha yetu ya Ukristo kutokuwa kamili na kama Daudi alivyosema:
Zaburi 11: 3;
Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini? (ZAB. 11:3 SUV).
Umuhimu mkubwa sana wa ubatizo unaenda tena kujidhihirisha katika maandiko haya yafuatayo:
I Yohana 5: 8, 9.
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. (1 YOH. 5:8, 9 SUV).
Mbinguni kuna watatu watakaotushuhudia na duniani pia kuna watatu watakaotushuhudia.
Kwa mbinguni watakuwa, Baba, Neno ambaye ni Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.
Duniani napo kutakuwa na watatu, Roho Mtakatifu, maji na Damu.
Roho Mtakatifu atakushuhudia kuwa amekujaza. Maji yatakushuhudia kuwa yalikubatiza na Damu itakushuhudia kuwa ilikuosha.
Usipuuzie swala la ubatizo. Najua umeoshwa kwa Damu ya Yesu, umejazwa na Roho Mtakatifu, lakini je, umebatizwa baada ya kuamini na tena kama maandiko yanavyofundisha kwa maji mengi?
Kama kuna mtu mmoja ambaye alikuwa hana ulazima wa kubatizwa, alikuwa ni Yesu Kristo maana katika siku Zake, ubatizo uliyokuwepo, yaani ule wa Yohana ulikuwa ni ubatizo wa toba. Watu walikuja kwa Yohana Mbatizaji kubatizwa, wakizitubia dhambi zao.
Mathayo 3: 5, 6.
Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao. (MT. 3:5, 6 SUV).
Kama watu walikuwa wanakuja kwa Yohana Mbatizaji kubatizwa huku wakizitubia dhambi zao, na ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, kulikuwa na umuhimu gani wa Yesu Kubatizwa wakati Yeye alikuwa Mwana Kondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu? Asiye na dhambi anahitaji vipi kubatizwa ubatizo wa toba?
Pia kwenye huo mstari hapo juu natamani uone kuwa walibatizwa huku wakiziungama dhambi zao. Kwamba umeongozwa sala ya toba haimaanishi usibatizwe, ungama na kubatizwa mpendwa wangu, ndo utaratibu wa kibibilia.
Yohana Mbatizaji alilijua hilo kuhusu Yesu na ndo maana Yesu alipokuja kwa Yohana kubatizwa, Yohana alikataa kumbatiza maana hakuona kwanini ililazimu Yesu kubatizwa. Kimsingi kwa mantiki ya ubatizo wa Yohana, Yesu hakuwa na ulazima wowote wa kubatizwa kwa ubatizo huo lakini bado hata hivyo alibatizwa.
Mathayo 3: 13 - 15.
Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. (MT. 3:13-15 SUV).
Ona maneno ambayo Yesu aliyasema, kubali hivi sasa, ndivyo ITUPASAVYO kutimiza haki yote.
Neno ITUPASAVYO ni neno la ufunguo sana katika huu mstari. Yesu hakusema INIPASAVYO, alisema ITUPASAVYO. Kila mmoja wetu inatupasa kubatizwa. Kama Yesu ambaye hakuhitaji kubatizwa alibatizwa mimi na wewe ni nani tujihesabie haki na kuona hatuwezi wala hatuhitaji kubatizwa?
Kama Yesu alitimiza haki yote kwa njia ya ubatizo, mimi na wewe ni nani tusiitimize haki yote pia kwa njia hiyo hiyo ya ubatizo?
Mtume Yohana katika waraka wake anazungumza jambo la muhimu na msingi sana.
I Yohana 2: 6.
Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. (1 YOH. 2:6 SUV).
Kama tunadai kuwa tunakaa ndani Yake basi imetupasa kuenenda kama Yeye alivyo enenda. Kama Yesu alibatizwa na tena kwenye maji mengi basi imetupasa nasi pia kubatizwa kama Yeye na tena katika maji mengi.
Mtume Petro kwenye waraka wake naye anafundisha:
I Petro 2: 21.
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. (1 PET. 2:21 SUV).
Yesu alituachia kielelezo tufuate nyayo zake. Kama alibatizwa nasi tufuate kielelezo chake na tubatizwe pia.
Pia Mtume Petro anasema tena katika waraka wake:
I Petro 3: 21.
Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. (1 PET. 3:21 SUV).
Haya maneno ya huyu mtume ni ya kina sana na ni muhimu yakizingatiwa. Anasema ubatizo unatuokoa siku hizi ila anakuwa makini sana kulisema kwa kina ili tusije tukaelewa vibaya tukafikiri ubatizo unaweza kuchukua nafasi ya Roho na Damu kama tulivyoona hapo awali. Ubatizo hauweki mbali uchafu wa mwili, hiyo ni kazi ya Damu ya Yesu, bali ni jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Kwa hiyo kusema kuwa ubatizo unatuokoa, anamaanisha kuwa una sehemu katika mchakato mzima wa wokovu wetu, ila sehemu yake kubwa ni kutupa jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Ndiyo maana kwa kila mmoja ambaye hajabatizwa baada ya kuamini na tena kwa maji tele, kila hili somo likizungumzwa, kujadiliwa, kufundishwa mbele zake anasikia dhamiri ikimchoma, maana hakuna namna mtu unaweza ukalipotezea jambo la muhimu kama hili, labda uamue tu kuchomwa dhamiri, usisikie tena.
Yesu alipokuwa anazungumza na Nikodemo kwa habari ya kuzaliwa mara ya pili, alisema maneno haya ambayo nayo ni ya muhimu sana kuzingatia:
Yohana 3: 3 - 5.
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. (YN. 3:3-5 SUV).
Yesu alikuwa anazungumza na Nikodemo kwa habari ya kuzaliwa mara ya pili na akamwambia wazi kabisa kuwa kuzaliwa mara ya pili ni kwa Roho na kwa maji.
Umezaliwa kwa Roho sawa, kwa maji je? Maana vyote viwili vinatakiwa ili kukamilisha kuzaliwa kwako mara ya pili na hapa Yesu dhahiri alipokuwa anazungumzia kuzaliwa kwa maji alikuwa anazungumza kuhusu ubatizo.
Haki ya Mungu inakiriwa kwa njia ya ubatizo na kupingwa kwa njia ya kukataa kubatizwa.
Luka 7: 29, 30.
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. (LK. 7:29, 30 SUV).
Ishara ya nje kuwa wote na watoza ushuru wameikiri haki ya Mungu ni kule kukubali kwao kubatizwa ubatizo wa Yohana. Ila Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao kwa kuwa hawakubatizwa naye. Je wewe umeikiri haki ya Mungu kwa kubatizwa kwa ubatizo aliyoagiza Yesu au wewe ni miongoni mwao wanaopinga shauri la Mungu juu yao kwa kukataa kubatizwa. Jihoji, pata jibu alafu chukua hatua.
Ili kujua kuwa ubatizo ulikuwa wa muhimu kiasi gani, sio tu Yohana ambaye alikuwa anabatiza lakini hata Yesu alipoianza huduma Yake akihubiri habari za Ufalme wa Mungu na toba, naye pia alikuwa anabatiza.
Yohana 3: 23, 26.
Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. (YN. 3:22, 26 SUV).
Yesu ni dhahiri kwa maandiko hayo hapo juu alikuwa akibatiza. Alienda Uyahudi na wanafunzi Wake, akashinda huko akibatiza. Kama ubatizo hauna umuhimu kiviile, Yesu anaendaje kushinda mahali akifanya zoezi ambalo halina umuhimu?
Aliyeshuhudiwa na Yohana Mbatizaji ng'ambo ya Yordani ni nani kama sio Yesu? Na hapa imeandikwa alikuwa anabatiza na wote walikuwa wakimwendea.
Kama Yesu alikuwa akibatiza mimi na wewe ni nani kusema kuwa sisi hatubatizi au kupinga ubatizo?
Yohana 4: 1, 2.
Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,) (YN. 4:1, 2 SUV).
Hili andiko latuonyesha kuwa Yesu mwenyewe binafsi hakuwa anabatiza bali wanafunzi wake ikimaanisha wazi kuwa walifundishwa na Yesu kubatiza. Ni huku kubatiza kulikuwa mchakato wa muhimu sana katika kuwafanya watu wanafunzi. Yesu alikasimu wajibu wa kubatiza kwa wanafunzi Wake, ili Yeye asije akajichosha kwa kufundisha, kufanya huduma kwa wagonjwa na waliyofungwa na juu yake kubatiza maelfu ya watu waliyokuwa wanamjia.
Yesu kwenye huduma Yake alibatiza, je mimi na wewe tunaweza kuwa zaidi Yake Yeye au tutafuata mfano Wake wa Kihuduma?
Tunafahamu kuwa Yohana Mbatizaji pia alipokuwa anabatiza watu aliwabatizia mto Yordani maana maji mengi yanahitajika kwa ajili ya kufanikisha na kukamilisha zoezi la ubatizo kibibilia.
Alionekana tena akibatiza watu mahali pengine na mahali hapo pengine palichaguliwa kama mahali pa kubatizia kwa kuwa kulikuwa na maji tele.
Yohana 3: 23.
Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. (YN. 3:23 SUV).
Ni dhahiri kabisa kwamba ubatizo ni kwa maji mengi na sio kwa kunyunyizwa, japo mimi sipingi ubatizo wa kunyunyizwa, ila sio uliyoagizwa na bibilia.
Katika mfano wa towashi wa Kushi, tunaona tena kuwa ubatizo ulikuwa ni wa maji tele sio wa kunyunyizwa.
Matendo 8: 36 - 39.
Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [ Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. (MDO 8:36-38 SUV).
Kama njiani walifika mahali penye maji, haya maji lazima yalikuwa tele na walipoyaona au towashi alipoyaona, akasema maji haya hapa nini kinanizuia nisibatizwe. Akaambiwa ukiamini kwa moyo wako wote inawezekana. Hii ni dhahiri kuwa hili tendo la ubatizo linafanywa baada ya mtu kuamini kwa moyo wake wote na sio kuna mtu anaamini kwa niaba yake. Kwa hiyo ubatizo wa watoto wafogo wasio na uwezo wa kuamini sio wa kibibilia hata kidogo na hata utaratibu wa baba na mama wa ubatizo sio wa kibibilia pia. Ni utaratibu tu wa kimapokeo katika makanisa yetu ambao mimi siupingi, ninasema una makusudi yake, sababu zake, madhumuni yake na malengo yake ila usichukuliwe kama mbadala wa ubatizo ambao Yesu aliuagiza au unaofundishwa na neno la Mungu. Tunaendelea kusoma towashi akikiri kuwa anaamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wakateremka wote wawili majini ambayo ni kiashiria kuwa hayo maji yalikuwa mengi, akabatizwa.
Ili kutambua kuwa ubatizo sio jambo la kufanya nao mzaha, ubatizo ni msingi mmojawapo wa agizo la Yesu. Kama Yesu aliona umuhimu wa kutoa agizo mahususi la kuweka ubatizo kama sehemu ya kutimiza wito mkuu au agizo Lake kuu kwetu, hatutakuwa tunaitendea haki hilo agizo tunapokuwa tunapuuzia swala la ubatizo.
Mathayo 28: 19, 20.
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (MT. 28:19, 20 SUV).
Agizo la Yesu la kuwafanya watu kuwa wanafunzi lina sehemu mbili, la kwanza likiwa kuwabatiza kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na la pili likiwa kuwafundisha kuyashika yote aliyotuamuru.
Hakuna namna unaweza kutimiza agizo kuu la Yesu bila ya kubatiza watu kama sehemu ya agizo hilo na hakuna namna unaweza kuwa mwanafunzi wa Yesu bila ya kubatizwa.
Yesu alisema maneno haya kuhusiana na mwanafunzi:
Mathayo 10: 24, 25.
Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? (MT. 10:24, 25 SUV).
Mwanafunzi hawezi kuwa zaidi ya Mwalimu wake. Yatosha mwanafunzi kuwa kama Mwalimu wake. Sisi kam wanafunzi wa Yesu, kama Yesu alibatizwa na alifundisha tubatizwe, sisi ni nani kutobatizwa au kuzuia watu wasibatize?
Lakini pia msisitizo unawekwa tena kwenye nukuu ya Marko ya agizo ambalo Yesu alilitoa kwa wanafunzi Wake:
Marko 16: 15, 16.
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. (MK. 16:15, 16 SUV).
Hivi maandiko yanaweza yakawa wazi zaidi ya hapa?
Tukaihubiri injili kwa kila kiumbe aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa. Umeamini nini kinakuzuia usibatizwe? Je ni mafundisho ya kidhehebu au ya kidini? Je ni mapokeo ya kidhehebu ndo yanakuzuia usibatizwe? Nakusihi kwa Jina la Bwana, pondeka nyenyekea ukabatizwe. Ni muhimu sana kuzingatia na kutii agizo la Yesu.
Umeamini moyoni mwako, umekiri kwa kinywa chako sasa kabatizwe ili kukamilisha mchakato mzima wa kuzaliwa kwako mara ya pili, ya kuokoka kwako.
Siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alipolishukia kanisa kwa mara ya kwanza, Petro baada ya kuhubiri ujumbe moto moto wa Injili, watu walichomwa mioyo. Tunasoma:
Matendo 2: 37 - 42.
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. (MDO 2:37-42 SUV).
Walipochomwa mioyo na ujumbe wakauliza wafanyaje, wakaambiwa watubu wakabatizwe kila moja wao kwa Jina la Yesu. Nataka uone hayo maneno, KILA MOJA, maana agizo hili ni kwa ajili ya kila mmoja wetu. Sote twatakiwa kubatizwa baada ya kuamini. Tunaendelea kusoma kuwa wale waliyolipokea neno lake walibatizwa. Wewe ushalipokea neno kwanini unakuwa mbishi kubatizwa? Au hujalipokea nini? Baada ya kubatizwa wakadumu katika fundisho la mitume kama Yesu alivyoagiza, batizeni alafu fundisheni. Sasa mbona wewe unaruka hatua muhimu? Umeamini alafu sasa unadumu katika mafundiaho bila ya kubatizwa. Haijakaa sawa hiyo.
Yule mkuu wa gereza la Filipi naye alitaka kujua yale yampasayo ili naye aokoke na alipopewa maelekezo tunaona naye na nyumba yake wote walibatizwa.
Matendo 16: 30 - 33.
kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. (MDO 16:30-33 SUV).
Wakati Petro alipokuwa yupo nyumbani kwa Cornelio akiwapelekea habari njema za wokovu wa Yesu, akiwa bado angali anahubiri walijazwa Roho Mtakatifu kwa ishara ya kunena kwa lugha mpya. Kilichofuata kinaonyesh umuhimu mkubwa ambao mitume waliweka kwenye swala zima la ubatizo na kwamba ubatizo sio kitu cha kupuuza na kuchukulia kiuwepesi.
Matendo 10: 44 - 48.
Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. (MDO 10:44-48 SUV).
Ndugu yangu, wewe unakataa kubatizwa kwa sababu tu umeshajazwa Roho Mtakatifu? Damu imekutakasa, Roho amekujaza, kwanini na maji yasikubatize?
Kama ulishawahi kubatizwa kwa utaratibu wa kanisa au dhehebu lako kabla ya kuamini haimaanishi usibatizwe baada ya kuamini. Soma pamoja nami mkasa huu ufuatao.
Matendo 19: 1 - 5.
Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. (MDO 19:1-5 SUV).
Alifika Efeso akakuta walikuwa wameshabatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Paulo hakuupinga alianisha tu dhumuni la ubatizo ule akawafundisha ule uliyoagizwa na Yesu na walipoelewa wala hawakubisha kubatizwa "tena" maana walielewa ule waliyobatizwa ulikuwa wa dhumuni gani na huu wa baada ya kuamini habari za Yesu una dhumuni gani. Tusikwepe ubatizo kwa mafundisho manyonge yasiyo na mzizi katika neno la Mungu.
Najua ulishabatizwaga ubatizo wa kanisani kwako ulipokuwa mtoto, hujaamini bado, ule una sababu yake ila sio huu ambao Yesu na bibilia wanaufundisha ambao mtu anabatizwa baada ya kuokoka.
Hili andiko lifuatalo labda linaweza kutufungua tuelewe vema:
I Wakorintho 10: 1, 2.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; (1 KOR. 10:1, 2 SUV).
Kama ambavyo wana wa Israel walibatizwa wawe wa Musa, tunaweza kubatizwa kuwa wa dhehebu fulani na pia tunaweza kubatizwa kuwa wa Yesu. Tusichanganye haya mambo.
Pia kuna watu nimeshawahi kuwasikia wakipinga swala la ubatizo kwa kusema Paulo alisema kuwa hakutumwa kubatiza.
Kwanza kabisa Paulo mwenyewe alibatizwa na Anania.
Matendo 9: 17, 18.
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; (MDO 9:17, 18 SUV).
Pili Paulo naye alibatiza.
Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine. (1 KOR. 1:14, 16 SUV).
Tunaona watu zaidi ya watatu hapa walibatizwa na Paulo mwenyewe, Krispo, Gayo na wa nyumbani mwa Stefana ambao hatuambiwi walikuwa wangapi alafu anamalizia kwa kusema zaidi ya hao sijui kama nilibatiza ye yote mwingine. Hakusema hakubatiza mwingine ni kwamba tu hakumbuki kama alibatiza mwingine. Na ndipo anasema hakutumwa yeye kubatiza.
I Korintho 1: 17.
Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika. (1 KOR. 1:17 SUV).
Kusema hivi haikumaanisha ubatizo ni mbaya au sio lazima bali ubatizo haukuwa sehemu ya msisitizo wa huduma ya Paulo.
Jambo la tatu ni kwamba kwenye agano jipya sijamwona mtu ambaye anafundisha kwa undani ubatizo na maana na faida zake kama Paulo kwenye nyaraka zake.
Kwa hayo tuliyoyapitia kwenye maandiko ni wazi kabisa ubatizo ni jambo lisilo kwepeka wala kuepukika.
NINI FAIDA NA UMUHIMU WA KUBATIZWA?
Ningependa sasa kumalizia somo langu hili na mafundisho yangu haya kwa kuangalia umuhimu na faida za kubatizwa na hapa tutaweka mkazo kwa kutumia maandiko kutoka katika nyaraka za mtume Paulo.
Warumi 6: 3 - 5.
Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; (RUM. 6:3-5 SUV).
Tunapobatizwa katika Kristo Yesu tunabatizwa katika mauti Yake. Tunapozamishwa ndani ya maji mengi ni ishara ya kuzikwa pamoja na Kristo katika mauti Yake, ili tunapotoka sasa kwenye hayo maji iwe ni ishara ya kuingia katika upya wa uzima kama ambavyo Yesu Naye alifufukuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba. Kubatizwa kunatuunganisha na mfano wa mauti Yake, ili tuje tuunganike Naye katika mfano wa kufufuka Kwake.
Kolosai 2: 12.
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. (KOL. 2:12 SUV).
Tunapobatizwa tunazikwa pamoja Naye katika ubatizo. Kila ambaye hajabatizwa hajazikwa pamoja Naye na kwanini upuuzie kitu cha muhimu hivi? Anaendelea kusema katika huo tumefufuliwa pamoja naye, katika huo nini? Ubatizo ndugu yangu, kwa kuamini nguvu za Mungu aliyemfugua katika wafu.
Kitendo cha kiishara cha kuzikwa pamoja naye na kufufuliwa pamoja naye kinatimizwa kupitia tendo la ubatizo.
Galatia 3: 27.
Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. (GAL. 3:27 SUV).
Tukibatizwa katika Kristo ni tendo ambalo linatupelekea kumvaa Kristo.
Kwa hiyo kimsingi tunaona kuwa ubatizo ni tendo la ishara la nje linaloonyesha kile ambacho kimefanyika ndani. Kwa hiyo kama tumekubali ya ndani tukubali na hili la nje pia.
Mungu akubariki sana.
Asomaye, afahamu.